Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Duh! Ile ndege ya Onana amelipiwa Sh250 milioni

Andre Onana Ndege Duh! Ile ndege ya Onana amelipiwa Sh250 milioni

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Manchester United imeripotiwa kulipa pesa nyingi sana kwa sababu tu ya kumsafirisha kwenye ndege ya kukodi, kipa wao Andre Onana kuwahi kujiunga na timu yake ya taifa ya Cameroon huko kwenye fainali za Afcon 2023 zinazoendelea kwa sasa Ivory Coast.

Onana alichelewa kujiunga na wenzake wa Simba Wasioshindika akisubiri aitumikie Man United kwanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Tottenham Hotspur, Jumapili iliyopita kabla ya kusafiri kwa ndege hiyo usiku kuwahi kujiunga na Cameroon, ambayo ilikuwa na mechi dhidi ya Guinea kwenye fainali hizo za Afcon 2023 siku iliyofuatia ya Jumatatu.

Hata hivyo, Onana alichelewa kucheza mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya 1-1 na badala yake alicheza mechi iliyofuatia na walikubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Senegal.

Kwa mujibu wa The Athletic, Onana aliondoka England Jumapili saa 10:30 usiku. Ndege aliyokodiwa ni ya kampuni ya VisaJet, ambayo inatoza kati ya Dola 12,000 na Dola 20,000 kwa kila saa utakalokuwa angani.

Na safari ya Onana ilikuwa ya saa nane, Hiyo ina maana kwa kiwango cha chini, Man United ililipia safari ya kipa huyo Dola 100,000, sawa na Sh250,792,000 za Kitanzania.

Onana usiku wa jana Jumanne, alitarajia kukaa golini kwenye mechi muhimu ya Cameroon dhidi ya Gambia, ilipokuwa ikihitaji ushindi mkubwa wa kukamatia tiketi ya kutinga hatua ya 16 bora ya fainali hizo za Afcon 2023, huku wakiomba, Senegal iichape Guinea.

Endapo kama Cameroon itakuwa imeshindwa kutinga hatua inayofuata, basi jambo hilo linaweza kumfanya Onana akaondoka mapema na kuwahi kwenye klabu yake ya Man United, ambayo Jumapili itakuwa na mchezo dhidi ya Newport County kwenye Kombe la FA.

Chanzo: Mwanaspoti