Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dube na Azam kuanza kupambana kuanzia kesho

Dube Na Azam Kuanza Kupambana Kuanzia Kesho.jpeg Dube na Azam kuanza kupambana kuanzia kesho

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji na wanachama ya TFF inakutana kesho Alhamisi tarehe 18 April 2024 kupitia mashauri tofauti tofauti ikiwemo sakata la mshambuliaji wa Azam FC PRINCE DUBE ambaye amaejiweka mbali na klabu hiyo akitaka kuondoka kwa madai mbalimbali yakiwemo ya kimkataba.

Habari ambazo Bin Kazumari inazo zinasema Dube aliiandikia TFF kulalamika kuhusiana na mkataba mpya wa Azam FC kwamba kuna vitu haviko sawa kwahiyo hautambui. Dube Ana mkataba na Azam FC ambao unaisha Julai 24 2024 na ndipo unapaswa kuanza mwingine wa miaka 2 mpaka Julai 2026.

Katika kesi hiyo itakayoanza kesho Alhamisi tarehe 18 April 2024 Azam FC watawakilishwa na wakili wa kimataifa kutoka Ureno na ameshawasiliana na TFF kuona uwezekano wa shauri la Prince Dube kufanyika kwa njia ya mtandao (zoom meeting) ili aweze kushiriki akiwa huko huko Ureno, wawakilishi wa Dube bado hatujafanikiwa kuwapata watatokea wapi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live