Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dube majanga mengine tena

7a7f58713e1875e69967455971417cb3 Dube majanga mengine tena

Thu, 11 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MSHAMBULIAJI wa Azam FC Prince Dube anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki mbili kufuatia kupata majeraha ya nyama za paja.

Dube aliumia katika mchezo dhidi ya Mwadui uliochezwa Shinyanga hivi karibuni na kutoka suluhu.

Kukosekana kwa mchezaji huyo aliyefunga mabao manane Ligi Kuu huenda kukawa pigo kwa wanalambalamba wa Chamazi, Azam FC kwa kuwa ni miongoni mwa washambuliaji tegemeo wa kikosi hicho.

Kwa mujibu wa daktari wa Azam FC, Mwanandi Mwankemwa nyota huyo atakuwa nje kwa wiki mbili kabla ya kurejea uwanjani tena kuitumikia timu yake.

"Dube atakuwa nje kwa muda wa wiki moja akiendelea na matibabu akipewa huduma na ile ya pili ataanza mazoezi mepesi kwa ajili ya kurejea katika ubora wake,”alisema.

Alisema baadaye atafanyiwa vipimo vingine ili kujua kama atakuwa amepona na kurejea katika mechi za ushindani.

Hii ni mara ya pili anaumia, aliwahi kuumia bega katika mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Yanga uliosababisha kupelekwa Afrika Kusini kwa upasuaji kisha akapona na kurejea dimbani.

Chanzo: www.habarileo.co.tz