Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dube kuwavaa Kagera Sugar

Dube Prince.jpeg Mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube

Fri, 3 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo anaweza akarejea uwanjani Alhamisi ijayo Azam FC ikimenyana na Kagera Sugar ya Bukoba.

Ni Azam FC ndio watakaokuwa wenyeji wa Kagera siku hiyo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Dube amekuwa nje kwa muda mrefu kutokana na maumivu na kukosekana kwake kumeipunguzia Azam FC idadi ya mabao mwanzoni mwa msimu.

Dube amekuwa na mwendelezo mzuri mazoezini kwa wiki ya tatu sasa na baada ya mazoezi mepesi kwa muda wote, jana alianza kujifua kikamilifu na wenzake katika programu kamili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live