Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dube kumuadhibu Katwila leo?

Prince Dube 1 E1599847429178 1024x640 Dube kumuadhibu Katwila leo?

Tue, 20 Oct 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By THOMAS NG'ITUMSHAMBULIAJI Prince Dube wa Azam Fc ndiye mshambuliaji tishio kwa sasa katika Ligi Kuu  Bara baada ya kufunga magoli sita na kuongoza katika chati ya wafungaji bora.

Dube leo atakuwa miongoni mwa washambuliaji watakaoingoza Azam katika mchezo wao dhidi ya Ihefu utakaopigwa kuanzaia saa 8:00 mchana katika uwanja wa Sokoine, Mbeya huku akitarajiwa kumuweka katika wakati mgumu kocha  mpya wa wapinzani wao, Zuberi Katwila .

Katwila amejiunga na timu hiyo Jumapili  akichukua nafasi ya Maka Mwalwisi aliyetupiwa virago na kibarua chake cha kwanza kitakuwa dhidi ya Azam leo.

Dube mwenye magoli sita, anakutana na  Ihefu ambayo imefunga mabao mawili tu kwenye ligi mpaka sasa huku ikiruhusu mabao manane.

Bila shaka Dube ndiye mchezaji ambaye anaweza kumpa kibarua kigumu leo kocha Katwila katika kikosi chake kwani ni mshambuliaji ambaye analijua goli huku akiwa na sifa ya kufunga mabao ya aina zote iwe kwa kichwa au kwa miguu.

Kocha msaidizi wa Azam Fc, Bahati Vivier amesema "Tunahitaji pointi tatu tu kila mechi.Unaweza kuiona jinsi gani kombinesheni ya Chirwa (Obrey), Djodi (Richard) na Dube (Prince)  ilivyo nzuri hivyo watakaokuja kuangalia mechi yetu watafurahia.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz