Hacheki nao. Ndio, mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube ameendeleza ubabe wake kwa Simba baada ya kuitungua tena katika sare ya bao 1-1, katika Dabi ya Mzizima, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
Ilikuwa pasi murua ya Paschal Msindo kutoka upande wa kushoto dakika ya 14 iliyotua kwa 'Mwanamfalme' aliyeteleza na kuuzamisha mpira nyavuni akimwacha kipa Ayoub Lakred.
Bao hilo lilidumu kwa dakika 90 kabla ya Clatous Chama kutibua furaha hiyo dakika za majeruhi ana kupeleka shangwe kwa mashabiki wa Simba.
Dube amekuwa na rekodi nzuri ya kuifunga Simba ikiwa ni mara ya tatu mfululizo kwenye Ligi Kuu Bara na mara moja kwenye Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).
Mshambuliaji huyo aliifunga Simba msimu uliopita kwenye nusu fainali ya ASFC Mei 7 na Ligi Kuu Februari 21, 2023 dakika ya 2 mchezo ulimalizika kwa sare ya 1-1 na kuichapa Simba 1-0 Octoba 21, 2022.