Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dube awataja Simba baada ya ushindi wao wa 5-0

Dube Awataja Simba Baada Ya Ushindi Wao Wa 5 0 Dube awataja Simba baada ya ushindi wao wa 5-0

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube amefunguka machache baada ya mchezo wao dhidi ya KMC mchezo ambao wameshinda goli tano kwa sifuri, ndani yake akawagusia Simba SC.

Amesema yeye anaangalia kwanza JKT ambao ndio mechi inayofuata, licha ya kukiri Simba ni timu kubwa.

"Simba ni timu kubwa, siwezi kuizungumzia kwa sasa akili yetu ni kwa JKT," alisema Dube.

Alipoulizwa kama atawafunga tena Simba kama ambavyo alifanya msimu uliopita, Dube alisema atapambana kufanya vizuri katika mchezo huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live