Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dube ana moto huyo! aisifu AFCON

Dube Prince.jpeg Mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube

Fri, 4 Feb 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube amesema licha ya timu yake ya taifa ya Zimbabwe kutofanya vizuri kwenye michuano ya Afcon amejifunza mengi na anaamini yatambeba katika mechi za Ligi Kuu Bara.

Dube aliiwakilisha nchi yake iliyokuwa Kundi B katika michuano hiyo inayoelekea ukingoni nchini Cameroon ikipangwa na nchi za Senegal, Guinea na Malawi na kumaliza mkiani ikiwa na pointi tatu.

“Tulikuwa kwenye kundi gumu lenye wachezaji wakubwa na wazoefu - wengi wao wanacheza timu kubwa za Ulaya, hivyo kuna vitu unajikuta unaiga kuanzia wanachofanya mazoezini mpaka kwenye mechi,” alisema Dube na kuongeza anarejea kuendelea alipoishia.

“Msimu niliuanza vibaya kutokana na majeraha. Niliumia sana kwa sababu malengo yalikuwa ni kuisaidia timu ila nashukuru nimerejea na nipo tayari kwa hilo.”

Kocha mkuu wa kikosi hicho, Abdihamid Moallin alisema, “Dube ni mshambuliaji ambaye kila kocha angetamani kuwa naye.”

Msimu uliopita Dube alimaliza akiwa na mabao 14.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz