Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dube aiua kikatili Yanga

Top Pic Data Dube aiua kikatili Yanga

Mon, 26 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na Azam umemalizika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa Azam kuibuka na ushindi wa bao 1-0, bao pekee likifungwa na Prince Dube dakika ya 86 .

Kipindi cha kwanza cha mchezo huo kilimalizika kwa suluhu huku nyota watatu wa Azam Raphael Bryson, Aggrey Moriss na Mudathir Yahya wakipata kadi za njano kwa kucheza faulo.

Kwa upande wa Yanga ni Michaerl Sarpong pekee aliyeoneshwa kadi ya njano baada ya kucheza madhambi kwenye kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili kilianza kwa Azam kulisakama lango la Yanga ndani ya dakika 10 za awali kabla ya Yanga kuamka na kuanza kusuka mipango ya kusaka bao.

Dakika ya 57, Yanga walifanya mabadiliko kwa kumtoa Deus Kaseke na nafasi yake kuchukuliwa na Ditram Nchimbi huku dakika 62 Azam wakimtoa Yahya Zayd na nafasi yake kuchukuliwa na Never Tigere.

Mabadiliko hayo hayakuonekana kubadili hali ya mchezo kwa timu zote mbili hadi dakika ya 69 Feisal alipoingia kwa upande wa Yanga akichukua nafasi ya Michael Sarpong.

Badiliko hilo lilionekana kuichangamsha Yanga hususani eneo la kiungo na kuanza kupandisha mashambulizi kuelekea lango la Azam licha ya kutopata bao.

Yanga waliendelea kufanya mabadiliko kwani dakika ya 78 walimtoa Carlos Calhinhos na nafasi yake kuchukuliwa na Haruna Niyonzima huku Azam nao wakijibu mapigo dakika ya 83 kwa kumtoa Ayoub Lyanga nafasi yake ikichukuliwa na Aziz Kader.

Dakika ya 86 straika wa Azam Prince dube akiwa nje ya boksi la 18 la Yanga alipiga kiki kali iliyomshinda kudaka kipa wa Yanga Farouk Shikhalo na kuzama nyavuni.

Ushindi huo unawafanya Azam kufikisha alama 54 wakisalia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi alama tatu nyuma ya Yanga walio na alama 57 nafasi ya pili.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz