Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dube aandika historia CAFCL

Dube 7098323 Prince Dube

Mon, 19 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Yanga ikiongoza kwa bao 3-0 dhidi ya Vital'O ya Burundi, mfungaji wao mshambuliaji Prince Dube amefunga bao la kwanza la mchezo huo na kuweka historia kupitia bao hilo.

Yanga inacheza dhidi ya Vital'O kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya mtoano wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika, mchezo unaopigwa kwenye Uwanja wa Azam complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Dube amefunga dakika ya tano tu ya mchezo huo lakini bao hilo limempa historia mpya akifunga bao la kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa tangu atue Tanzania.

Dube amefunga bao hilo kwenye mchezo wake wa kwanza wa Kimataifa wa kimashindano, akisajiliwa na Yanga msimu huu akitokea Azam aliyoitumikia kwa miaka minne tangu atue nchini

Dube ambaye alitua Tanzania mara ya kwanza 2020 akiletwa na Azam hakuwahi kucheza Ligi ya Mabingwa akiandika historia hiyo akiwa na Yanga.

Mshambuliaji huyo raia wa Zimbabwe amefunga bao Moja pekee kwenye mashindano ya Afrika akiwa na Azam akifunga Bahir Dar Kenema, kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita, Azam ikilazimishwa sare ya mabao 2-2 kisha kutolewa kwa matuta 4-3 na Waethiopia hao.

Amkumbuka mke wa bosi

Wakati Dube akifunga bao hilo akaonyesha fulana yake ya ndani ikiandikwa maneno ya 'Happy birthday Boss of the Boss' akimtakia heri ya kuzaliwa mke wa Mfadhili na Bilionea wao Gharib Said Mohammed ambaye Jana alikuwa akikumbuka siku yake ya kuzaliwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live