Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dube: Tuzo ya MVP apewe Fei Toto

Prince Dube Ms Dube: Tuzo ya MVP apewe Fei Toto

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji, Prince Dube ameshindwa kujizuia na kuweka bayana Mchezaji Bora msimu huu wa Ligi Kuu ni Feisal Salum Feitoto na kutoa sababu za kumpa tuzo nyota huyo wa Azam FC anayeongoza kwa mabao akilingana na Aziz Ki Yanga.

“Ukiachana na mabao 18 aliyonayo Feitoto, aina ya uchezaji wake wa kupiga mashuti, aina ya pasi zake anazotoa kwa wachezaji wenzake, nidhamu yake uwanjani ni kubwa si mchezaji ambaye ni mgovi,” alisema Dube na kuongeza;

“Sina maana viungo wengine ni wabaya, ila kwa upande wangu, aliye bora zaidi msimu huu ni Feitoto na anastahili kabisa kubeba tuzo. Mbali na yeye, kwa upande wa kipa aliyenivutia zaidi Djigui Diarra wa Yanga, kwani amefanya makubwa na kutumia ujuzi mkubwa awapo uwanjani.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live