Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dube Aipa Jeuri Azam, Lyanga Nje Miezi Miwili

Prince Dube Dube Aipa Jeuri Azam, Lyanga Nje Miezi Miwili

Tue, 30 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

HABARI njema kwa mashabiki wa Azam ni kurejea na kuanza mazoezi kwa mshambuliaji wao Mzimbabwe Prince Dube aliyekosekana kwa muda mrefu, huku chungu nyingine ikiwa ni ile ya kukosekana kwa kiungo mshambuliaji wao Ayoub Lyanga kwa muda wa miezi miwili.

Dube amekosekana uwanjani tangu mwezi Mei mwaka huu kutokana na tatizo la tumbo alilolipata kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Rhino Rangers, Lyanga yeye Novemba 16, mwaka huu alifanyiwa upasuaji wa mfupa wa meno ya juu nchini Afrika Kusini kufuatia majeraha aliyoyapata katika mchezo dhidi ya Geita Gold.

Mkuu wa Kitengo cha habari na mawasiliano wa Azam, Zakaria Thabith alisema: “Taarifa njema kwa mashabiki wa Azam ni kuwa mshambuliaji wetu Mzimbabwe, Prince Dube anaendelea vizuri na mazoezi baada ya kuwa nje ya Uwanja kwa muda mrefu akiuguza majeraha na hivi karibuni atarejea kwenye majukumu yake uwanjani.

“Kuhusiana na Lyanga yeye baada ya kufanyiwa upasuaji Novemba 16, mwaka huu anatarajiwa kukosekana uwanjani kwa kipindi kisichopungua miezi miwili, anaendelea na taratibu za matibabu na hali yake inazidi kuimarika kila siku.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live