Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Droo ya Carabao imepangwa kimchongo?

Kombe La Carabao Pic Carabao Cup

Fri, 22 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashabiki wa soka wamelalamika kuwa droo ya nusu fainali ya Kombe la Carabao imepangwa makusudi kimchongo ili Liverpool na Chelsea zisikutane katika hatua hiyo.

Liverpool iliibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya West Ham katika mchezo wa robo fainali, hivyo imepangiwa kucheza na Fulham, kwenye mechi ya nusu fainali, wakati Chelsea itamenyana na Middlesbrough inayonolewa na kiungo wa zamani wa Manchester United, Michael Carrick.

Chelsea ilitinga fainali ya Kombe la Carabao baada ya kuiondoa Newcastle kwa mikwaju ya penalti 4-2 kwenye mechi ya robo fainali. Hata hivyo, mashabiki wa soka waliibuka mitandaoni na kuponda kuwa droo ya Carabao haikubaliki wakidai imepangwa kimchongo.

Kulikuwa na nafasi ya asilimia 33, Chelsea na Liverpool zikutane nusu fainali hata hivyo kocha Mauricio Pochettino akabahatika kupangiwa timu moja inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (Championship).

Hata hivyo, Mashabiki wenye hasira waliopinga droo ya Carabao, wakaandika maoni yao mitandaoni.

"Droo ya Carabao imepangwa kimchongo kabisa ili timu kubwa zikutane fainali. Middlesborough na Fulham sidhani kama zina nafasi."

Shabiki wa tatu akaandika: "Droo ya Fulham na Middlesbrough." Shabiki wa nne akaandika: "Hii ni sapraizi kwa Liverpool na Chelsea, nadhani wadhamini watafarijika."

Shabiki wa mwisho akamaliza kwa kusema: "Ningefurahi kuweka Pauni 1,000 kwa ajili ya droo. Imepangwa fainali ya Liverpool na Chelsea."

Endapo Liverpool na Chelsea zitacheza fainali kama ilivyotarajiwa, itajirudia fainali ya Kombe la Carabao mwaka 2022 ambayo kikosi cha Jurgen Klopp kilibeba.

Liverpool inafukuzia taji hili kwa mara ya tisa wakati Chelsea imebeba mara tano katika historia ya klabu yao.

Wakati huo huo, Middlesbrough iliwahi kubeba mwaka 2004 baada ya kuifunga Bolton, wakati Fulham ikitinga nusu fainali kwa mara ya kwanza katika historia yao baada ya kuiondoa Everton kwa mkwaju wa penalti 7-6.

Nusu fainali itachezwa kuanzia Januari 8 hadi Januari 22 kabla ya fainali itakayochezwa Februari 25 kwenye Uwanja wa Wembley.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live