Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Droo ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa kufanyika Jumatatu ijayo

Droo Ya 16 Bora Ligi Ya Mabingwa Kufanyika Jumatatu Ijayo Droo ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa kufanyika Jumatatu ijayo

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Droo ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa itafanyika Jumatatu, Disemba 18, huku klabu mbili za Uingereza zikisubiri kujua hatima yao.

Mabingwa Manchester City, na Arsenal, walishinda makundi yao na kutinga hatua ya mtoano, huku Newcastle, Manchester United na mabingwa wa Uskoti Celtic wakijipata nje.

Ni nani aliyefuzu? Waliowekwa kwenye makundi: Arsenal, Atletico Madrid, Barcelona, Bayern Munich, Borussia Dortmund, Manchester City, Real Madrid, Real Sociedad.

Ambao hawajawekwa: Copenhagen, Inter Milan, Lazio, RB Leipzig, Napoli, Paris St-Germain, Porto, PSV Eindhoven.

Droo ni lini na itafanyika wapi? Droo ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa itafanyika Jumatatu, Disemba 18 saa 11:00 GMT katika ukumbi wa House of European Football huko Nyon, Uswizi.

Droo hufanywaje? Kila mshindi wa kundi atatolewa na kupangwa dhidi ya timu iliyoshika nafasi ya pili katika kundi jingine, ambao wote hawajapatikana. Timu haziwezi kuwekwa dhidi ya klabu zinazotoka nchi moja, au timu zilizokuwa kundi moja nazo.

Mechi za 16 bora zinachezwa lini? Mechi za mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora zitachezwa kwa wiki mbili, 13-14 na 20-21 Februari 2024, na marudiano 5-6 na 12-13 Machi.

Droo za robo fainali na nusu fainali zitafanyika kwa pamoja Ijumaa, Machi 15.

Jinsi hatua ya makundi ilivyomalizika

Manchester United walimaliza wa mwisho katika Kundi A baada ya vipigo vinne kutoka kwa mechi sita za kundi hilo.

Ilikuwa ni mara ya sita kwa Mashetani Wekundu kushindwa kutinga hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na mara ya kwanza kumaliza mkiani mwa kundi lao tangu 2005-06.

Bayern Munich walitinga hatua ya 16 bora wakiwa washindi wa kundi wakiwa na mechi mbili zilizosalia, huku Copenhagen ikisonga mbele kwa awamu ya muondoano kwa mara ya kwanza tangu 2010-11.

Galatasaray ilitolewa katika raundi ya muondoano ya Ligi ya Europa.

Arsenal walishinda kundi lao wakiwa na mchezo mmoja wa ziada na PSV Eindhoven pia wakimaliza katika nafasi ya pili baada ya mechi tano.

Lens iliepuka kushindwa na Sevilla katika mechi yao ya mwisho ili kujihakikishia nafasi ya kucheza Ligi ya Europa.

Real Madrid ilifika hatua ya mtoano kwa msimu wa 26 mfululizo, ikikamilisha Kundi C ikiwa na rekodi kamili ya ushindi sita kutoka mechi sita.

Napoli walipata nafasi ya pili kwa ushindi dhidi ya Sporting Braga siku ya sita ya mechi, huku timu ya Ureno ikishuka hadi kwenye Ligi ya Europa.

Union Berlin ilimaliza wa mwisho katika Kundi C katika msimu wao wa kwanza katika mashindano hayo.

Real Sociedad wameongoza Kundi D mbele ya Inter Milan kwa tofauti ya mabao.

Benfica walichukua nafasi ya tatu kutoka kwa Red Bull Salzburg baada ya dakika za lala salama pale Arthur Cabral alipowafungia na kuwapa ushindi wa mabao 3 kwa moja .

Atletico Madrid iliifunga Lazio 2-0 katika mchezo wa fainali na kumaliza ya kwanza katika kundi hilo.

Feyenoord wanashuka kwenye Ligi ya Europa na Celtic wametoka kwenye mashindano hayo.

Newcastle walikuwa wamebakisha dakika 45 kutoka kwa hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa, lakini waliishia kuondoka kabisa kwa kuchapwa 2-1 nyumbani na AC Milan, ambao waliwatoa kwenye Ligi ya Europa.

Borussia Dortmund ilimaliza kileleni mwa Paris St-Germain baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wao wa mwisho.

Washindi wa kundi Manchester City na washindi wa pili RB Leipzig walifika hatua ya 16 bora zikiwa zimesalia mechi mbili.

Young Boys walimaliza wa tatu na Red Star Belgrade walikosa kushinda mechi yoyote.

Barcelona wako katika awamu ya muondoano kwa mara ya kwanza katika misimu mitatu.

Porto iliungana nao katika hatua ya 16 bora kwa ushindi wa 5-3 dhidi ya Shakhtar Donetsk, ambao walimaliza katika nafasi ya tatu.

Royal Antwerp ilimaliza ya mwisho.

Chanzo: Bbc