Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Droo Ligi ya Mabingwa Ulaya 2024/25

Iugwdiudd Droo Ligi ya Mabingwa Ulaya 2024/25

Thu, 29 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kumekucha. Droo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itapangwa leo Alhamisi, huku mashabiki wa Arsenal wakiwa kwenye hofu kubwa ya chama lao kupangwa na vigogo kwenye mikikimikiki hiyo.

Michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu wa 2024/25 itafanyika kwa mara ya kwanza kuzingatia mfumo mpya tofauti na zamani.

Mfumo wa zamani wa michuano hiyo inayoshirikisha timu 32, ambazo zilikuwa zikipangwa kwenye makundi manane yenye timu nne kila mmoja, ambao ni mtindo ulioanza tangu 1967, sasa umekuwa zilipendwa na Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu 2024-25 itakuwa ya kitofauti kabisa.

Na sasa timu zitakazoshiriki ni 36 na hazitapangwa kwenye makundi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Timu hizo 36 zitachuana kwa mtindo wa ligi, ambapo kila timu itacheza mechi nane ili kutambua hatima yao kwenye kuvuka hatua inayofuata na kuingia kwenye mtoano wa mikikimikiki hiyo ya kusaka ubingwa wa Ulaya.

Kwa mtindo huo mpya, kila timu itacheza mechi nne nyumbani na mechi nne nyingine ugenini. Na kwamba kwenye upangaji wa droo hiyo, timu hizo zitawekwa kwenye vyungu vinne na kila timu itacheza na wapinzani wawili kwenye kila chungu kimoja.

Timu nane za juu zitafuzu moja kwa moja kwenye hatua ya mtoano ya 16 bora, wakati timu itakayokuwa kwenye nafasi ya tisa hadi 24, zitacheza mchujo wa mechi mbili nyumbani na ugenini ili kupata nane nyingine zitakazokamilisha idadi ya timu hizo 16 kwenye hatua ya mtoano.

Timu ambayo itashika nafasi ya 25 kwenda chini, zitakuwa zimetupwa nje kwenye michuano hiyo na hazitahamia kwenye michuano ya Europa League, tofauti na ilivyokuwa kwenye mfumo wa zamani, ambapo timu ambazo zinashindwa kuvuka kwenye hatua ya makundi, zile ambazo zilizokuwa zikimaliza nafasi ya tatu kwenye makundi yao, zilikuwa zikihamia kwenye michuano hiyo ya ngazi ya pili kwa ukubwa huko Ulaya.

Mchakato wote wa droo hiyo utapangwa leo, Alhamisi huko Monaco, Ufaransa. Wasiwasi uliopo ni kwamba Arsenal inaweza kujikuta kwenye wakati mgumu wa kupangiwa timu ngumu tupu.

Kimsingi, Arsenal inatarajia kuwa kwenye Chungu Namba 2 kwenye droo hiyo na kujiweka kwenye hatari ya kukutana na miamba ya Ulaya, Bayern Munich na Real Madrid, Paris Saint-Germain, Juventus, Sporting Lisbon na PSV Eindhoven, ambao ni miamba mingine yenye uwezekano wa kupangwa kucheza na kikosi hicho cha kocha Mikel Arteta kwenye michuano hiyo ya Ulaya.

Na inatabiriwa pia Arsenal inaweza kucheza na mshindi wa mechi ya mchujo kati ya FC Midtjylland na Slovan Bratislava.

Arsenal ilifika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita ikiwa ni mara ya kwanza baada ya kutokuwapo kwenye michuano hiyo kwa miaka mitano. Kikosi hicho cha kocha Arteta kilitupwa nje ya michuano hiyo na Bayern, baada ya kuchapwa kwa jumla ya mabao 3-2.

Timu ambazo Arsenal inaweza kupangwa kucheza nazo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu ni pamoja na Bayern, Real Madrid, PSG, Juventus, Sporting Lisbon, PSV, FC Midtjylland au Slovan Bratislava na Sturm Graz.

Miamba mingine ya Ligi Kuu England, Aston Villa - timu ambazo inaweza kupangwa nazo kwenye michuano ni pamoja na Atletico Madrid, Inter Milan, Bayer Leverkusen, Atalanta, Feyenoord, Celtic, Bodo/Glimt au Red Star Belgrade na Monaco.

Liverpool inaweza kupangwa kuchuana na Borussia Dortmund, RB Leipzig, Benfica, Club Brugge, Young Boys au Galatasaray, Malmo au Sparta Prague, Bologna na Girona, wakati Manchester City inaweza kucheza na Barcelona, AC Milan, Shakhtar Donetsk, Lille au Slavia Prague, Dynamo Kyiv au RB Salzuburg, Stuttgart, Dinamo Zagreb au Qarabag na Brest.

Chanzo: Mwanaspoti