Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Drogba ampasua bosi wa Chelsea

Drogba Ashauri Wachezaji Kufanyiwa Vipimo Baada Ya Kifo Cha Sylla Didier Drogba

Thu, 20 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gwiji wa Chelsea, Didier Drogba amewashutumu wamiliki wa sasa wa klabu hiyo kwa kukosa daraja na kusisitiza kuwa ‘haitambui’ Chelsea tena.

Real Madrid ilimaliza msimu wa Chelsea kwa kuwatupa nje ya Ligi ya Mabingwa kwa ushindi wa 2-0 (agg 4-0) Uwanja wa Stamford Bridge Jumanne usiku.

Mmiliki mwenza Todd Boehly ametumia paundi milioni 600 tangu achukue nafasi hiyo Mei 2022 lakini utawala wake umekuwa wa majanga hadi sasa.

“Niliijua klabu hii ikiwa na daraja fulani enzi za Abramovich, lakini leo naiona haipo. Ni ngumu sana kwangu kuona jinsi walivyowaondoa watu fulani,” alisema Drogba.

“Wanapaswa kurudi kwenye kanuni na maadili waliyokuwa nayo. Siitambui klabu yangu. Sio klabu moja tena, kuna mmiliki mpya na maono mapya.

“Ni kweli tunajaribu kulinganisha na kile kilichotokea wakati wa (Roman) Abramovich ambapo wachezaji wengi waliletwa, lakini maamuzi yalikuwa ya akili sana.

“Kuleta wachezaji kama Petr Cech, Andriy Shevchenko, Hernan Crespo, Micheal Essien, Florent Malouda, na mimi Ilifanyika ili kushinda mataji.

“Ni wachezaji wenye uzoefu fulani lakini mkakati sasa ni tofauti, tunaweka dau kwa wachezaji wachanga. Lakini chumba cha kubadilishia cha wachezaji zaidi ya 30 ni vigumu [kusimamia] kwa meneja.

“Wanakosa viongozi wenye mvuto. Unahitaji wachezaji wanaocheza mchezo, wanaochukua majukumu yao. Unahitaji mchezaji ambaye analeta wazimu kidogo kwenye uwanja.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: