Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Drogba, Mane kunogesha droo za AFCON

Mastaaaaaaaaaa Drogba, Mane kunogesha droo za AFCON

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mastaa wa soka Afrika, Didier Drogba, Sadio Mane, Obi Mikel na Achraf Hakimi watakuwa sehemu ya kusapoti upangaji wa makundi leo ya Fainali za Mataifa Afrika (Afcon) zitakazofanyika mwakani.

Droo hiyo itafanyika Abidjan nchini Ivory Coast saa 1:00 usiku kwa saa za huko huku ikiwa ni saa 4:00 usiku kwa hapa nyumbani.

Drogba ni mfungaji bora wa timu ya Taifa Ivory Coast akiifungia timu hiyo mabao 65 katika mechi 105 huku akikumbukwa kwa kufunga bao la kwanza katika kombe la Dunia 2006 akiwa na timu hiyo. Drogba amefunga mabao 11 katika mechi 24 za Afcon na ameisaidia timu hiyo kucheza fainali za kombe hilo 2006 na 2012.

Wakati huohuo mchezaji mwenzake wa zamani Chelsea, Mikel yeye 2013 alichukua kombe la Afcon akiwa na kikosi cha Nigeria kisha mara tatu alichukua medali ya mshindi wa pili.

Upande wa Sadio Mane, yeye alifunga bao la penalti ambalo lilikuwa la kwanza pale Cameroon 2021, pia alitajwa kama mchezaji bora wa Afrika mara mbili. Mane ndio mfungaji bora wa muda wote kwenye timu hiyo akifunga mabao 38 katika mashindano na upande wa Afcon alifunga mabao nane kwenye mechi 18.

Hakimi ambaye ni beki wa Paris Saint Germain (PSG), ambaye ni mchezaji wa Morocco yeye ametengeneza rekodi ya kuingia nusu fainali katika kombe la Dunia 2022.

Timu zilizopo kwenye droo hizo ni Ivory Coast, Algeria, Angola, Burkina Faso, Cameroon, Cape Verde, Congo DR, Egypt, Equatorial Guinea, Gambia, Ghana, Guinea, Guinea-Bissau, Mali, Mauritania, Morocco, Mozambique, Namibia, Nigeria, Senegal, South Africa, Tanzania, Tunisia na Zambia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live