Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dortmund yatepeta kwa Ajax

Ajax Dortmund vs Ajax

Thu, 4 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Huenda wengi wasiamini matokeo wanayopata Borussia Dortmund mbele ya wababe wa Soka la Uholanzi timu ya Ajax,

Baada ya kupokea kichapo cha magoli 4-0, mchezo wa kwanza waliokutana hatua ya makundi, usiku wa jumatano Dortmund wakiwa nyumbani wamekubali tena kipigo cha magoli 3-1 kutoka kwa Ajax.

Mchezo huo wa Kundi C, umewapa nafasi Ajax kuongoza kundi kwa alama 12, wakifuatiwa na Dortmund wenye alama sita, Sporting CP nayo ikiwa nafasi ya tatu ikiwa na alama sita huku Beskitas wakiburuza mkia wakiwa hawana pointi hata moja huku kila timu ikiwa imekwishacheza michezo minne.

Dortmund ndio waliokuwa wa kwanza kupata goli, lililowekwa kimiani na Marco Reus kwa mkwaju wa Penati dakika ya 37.

Ajax wamepata magoli yao kupitia kwa D. Tadic 72',S. Haller 83 na D. Klaassen mnamo dakika ya 90+3.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live