Borussia Dortmund imekamilisha uhamisho wa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast na Ajax, Sebastien Haller.
Takribani Euro milioni 31 zimetumika kufanikisha usajili wa Haller mwenye umri wa miaka 28 ambapo bila shaka anakuwa mrithi wa Erling Braut Haaland.
Haller anarudi tena Ujerumani kwani mwaka 2017-2019 alicheza Eintracht Frankfurt.
Akizungumza baada ya kukamilisha uhamisho wake amesema anategemea mapokeo makubwa kutoka kwa mashabiki wa Dortmund takribani 80,000.
Anaondoka Ligi ya Uholanzi baada ya miezi 11 akiwa amefunga jumla ya magoli 47 katika mechi 66, bao 11 zikifungwa kwenye msimu uliopita wa Uefa.