Borussia Dortmund wamelazimika kutumia nguvu ya ziada kuibuka na ushindi mgumu wa bao 4-3 dhidi ya Augsburg katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Ujerumani Bundesliga baada ya siku 72 tangia kusimama.
Nyota wa England Jude Bellingham alifunga bao lake la nne kwenye Ligi msimu huu. Augsburg walitokea nyuma goli moja mara tatu kabla ya Dortmund kupata ushindi kupitia bao Safi la volley lake Giovanni Reyna.
Kinda Bynoe-Gittens aliifungia Dortmund la tatu kabla la David Colina kufanya mambo kuwa 3-3, kisha Reyna akiwa kwenye mchezo mzuri aliweza kufunga bao lingine akimalizia pasi ya Bellingham.
Arne Maier alisawazisha kabla ya beki Nico Schlotterbeck kujikuta wenyeji wakiongoza tena.
Matokeo hayo yanaifanya Dortmund wanakwea alama saba nyuma ya vinara Bayern Munich.