Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dortmund yaangukia kwa Ziyech

Ziyech Ushauri Mchezaji wa Chelsea, Hakim Ziyech

Sat, 13 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kulingana na majarida mbalimbali ya michezo barani ulaya, winga wa Chelsea, Hakim Ziyech anaweza kuondoka Stamford Bridge katika dirisha la usajili la mwezi January na kujiunga na Borussia Dortmund ya Ujerumani.

Ziyech alijiunga na Chelsea mwaka 2020 kwa ada ya £38 million akitokea Ajax ya Uholanzi baada ya kufanya vizuri kwa misimu kadhaa.

Ziyech amekuwa akisumbuliwa na majeraha tangu ajiunge na Chelsea, huku akipata changamoto kuingia katika kikosi cha kwanza mbele ya Odoi, Christian Pulisic, Kai Havertz na Timo Werner.

Kulingana na Jarida la Bild kutoka Ujerumani limeripoti klabu ya Borussia Dortmund wapo tayari kumsajili mchezaji huyo kwa mkopo katika majira haya ya baridi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live