Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dortmund wakomaana na Jude Belligham

Jude Bellingham Hg Jude Bellingham

Tue, 14 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Borussia Dortmund ina matumaini makubwa ya kumbakiza nyota wake ndani ya klabu hiyo kiungo wa kimataifa wa Uingereza Jude Bellingham ambaye amekua akifukuziwa na vilabu mbalimbali barani ulaya.

Kupitia mkurugenzi wa michezo ndani ya klabu ya Borussia Dortmund Sebastian Kehl amezungumza na kusema anafikiri kiungo Jude Bellingham anaweza kusaini mkataba mpya wa kuitumikia klabu hiyo kwa miaka mingine licha ya changamoto wanazokutana nazo.

Kiungo Jude Bellingham mwenye umri wa miaka 19 amekua kwenye ubora mkubwa sana ndani ya klabu hiyo tangu alipojiunga klabuni hapo, Vilabu kadhaa barani ulaya vimekua vikihitaji saini ya kiungo huyo ambaye anafanya vizuri kunako ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga.

Mkataba wa Kiungo huyo unamalizika mwaka 2025 lakini inaelezwa klabu hiyo inaweza kumuuza dirisha lijalo la usajili ili kuweza kupata kiasi kikubwa cha fedha, Lakini mkurugenzi huyo ameweka wazi kua matumaini yao ni kiungo huyo kusaini mkataba mpya ili aweze kusalia ndani ya klabu ya Borussia Dortmund kwa muda mrefu zaidi.

Klabu ya Real Madrid inatajwa kuiwinda kwa ukaribu zaidi saini ya kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza kwenye dirisha kubwa lijalo bila kuisahau klabu ya Manchester United, Borussia Dortmund watakua na kazi kubwa sana ya kumshawishi kiungoo huyo kusalia klabuni hapo mwishoni mwa msimu kutokana na vita watakayokumbana nayo kutoka kwa vilabu vikubwa barani ulaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live