Borussia Dortmund ikiwa na Sebastien Haller imeichapa bao 5-1 klabu ya Freiburg katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Ujerumani Bundesliga mchezo ambao Sébastien Haller amefunga bao la kwanza akirejea baada ya kuwa nje kwa muda sasa.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alifunga bao la tatu kwenye ushindi huo ambao mabao mengine yamefungwa na Nico Schlotterbeck, Karim Adeyemi, Julian Brandt na Gio Reyna.
Holer alifunga bao la kufutia machozi kwa Freiburg ambayo ilimaliza mchezo wakiwa pungufu kufuatia Sildillia kuonyeshwa kadi nyekundu.
Haller aliposajiliwa na Dortmund kutokea Ajax alilazimika kufanyiwa upasuaji mara mbili kutokana na matatizo ya kansa lakini sasa anaonekana kuwa sawa baada ya kurejea uwanjani Januari 22.
Matokeo hayo yanaifanya Dortmund kukaa nafasi ya tatu alama mbili nyuma ya vinara Union Berlin.