Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dortmund na Chelsea, kuna dili kwa Hakim Ziyech?

Ziyech Na Tuchel Hakim Ziyech akiwa na Thomas Tuchel

Wed, 15 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Borussia Dortmund inaripotiwa kuwa inataka kujaribu kufukuzia saini ya nyota wa Chelsea Hakim Ziyech.

Katika msimu ambao amekuwa akipambana na majeraha, Ziyech amecheza mechi 11 huku mechi tano akitokea benchi katika mashindano yote.

Hata hivyo, taarifa zinabamba zaidi kuwa Mmorocco huyo anatatizwa na kukosa muda wa kutosha wa kucheza katika kipindi cha kwanza cha msimu.

Kwa mujibu wa Bild, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ‘hajaridhishwa’ na hali yake Stamford Bridge na yuko tayari kuondoka the Blues.

Dortmund inadaiwa kumtambua Ziyech kama kipaumbele chao mwezi Januari huku wakitaka kupambana na vinara wa Bundesliga Bayern Munich.

Hata hivyo. bila kujali kama ni dili la kudumu au la mkopo kwa Ziyech, kocha mkuu wa Chelsea Thomas Tuchel anatarajiwa kukataa kutengana na mchezaji huyo ambaye amemsifu sana katika wiki za hivi karibuni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live