Klabu ya Borussia Dortmund inayoshiriki Ligi kuu nchini Ujerumani unaweza ukasema kuwa haifanyi biashara kwa hasara kutokana na kuwanunua wachezaji wake kwa bei nafuu na kuwauza kwa bei mbaya.
Ifuatayo ni orodha ya wachezaji iliyowanunua kwa bei ndogo na kuwauza kwa faida kubwa na maisha yanaendelea.
▪︎Ousmane Dembele alinunuliwa kwa Euro Milioni 15 akauzwa kwa Barcelona Euro Milioni 105 .
▪︎Pierre Aubameyang alinunuliwa kwa Euro Milioni 13 akauzwa kwa Arsenal kwa Euro Milioni 63.
▪︎Christian Pulisic alinunuliwa kwa Euro laki mbili na nusu akauzwa kwa Chelsea kwa Euro Milioni 64.
▪︎Jadon Sancho alinunuliwa kwa Euro Milioni 8 na akauzwa Manchester United kwa Euro Milioni 85.
▪︎Erling Braut Haaland alinunuliwa kwa Euro Milioni 20 na anauzwa Man City kwa Euro Milioni 60.
Borussia Dortmund ilitumia Euro Milioni 56 kuwanunua nyota hao na ikawauza kwa jumla ya Euro Milioni 377 na kutengeneza faida ya Euro Milioni 321.