Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dominic Calver-Lewin azigonganisha Newcastle, Man United

Calvert Lewin Man Dominic Calver-Lewin

Sun, 14 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Newcastle inataka kuingia katika vita dhidi ya Manchester United kwa kutuma ofa nyingine kwenda Everton kwa ajili ya kuipata saini ya straika wa timu hiyo Dominic Calvert-Lewin, 27, katika dirisha hili.

Mabosi wa Newcastle wameshawishika kutaka kumsajili Lewin baada ya kuibuka kwa taarifa kwamba mazungumzo yake na Everton juu ya kuongeza mkataba mpya yamegonga mwamba.

Man United ambayo inataka kuboresha eneo lao la ushambuliaji imekuwa ikitajwa kutaka kumsajili Lewin kwa muda mrefu.

Mkataba wa sasa wa staa huyo unatarajiwa kumalizika mwaka 2025, msimu uliopita alicheza mechi 38 za michuano yote na kufunga mabao nane.

Everton ipo tayari kumuuza Lewin kwa sababu inahofia kumpoteza bure ifikapo mwisho wa msimu ujao ama akaondoka kwa kiasi kidogo Januari mwakani.

Chanzo: Mwanaspoti