Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dogo wa miaka 16 aweka rekodi Liverpool

Trey Nyoni.jpeg Dogo wa miaka 16 aweka rekodi Liverpool

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dogo Jina lake anaitwa Trey Nyoni umri wake ni miaka 16 usiku wa Jana ameandika rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi katika klabu ya Liverpool kucheza Kombe la FA.

Liverpool imemsajili bwana mdogo kwa mipango ya muda mrefu baada ya kuondoka kwa Jordan Henderson na Fabinho ambao wameenda Saudi Arabia.

Mjadala mkubwa baada ya kuonekana ni asili ya dogo kutokana na jina lake la mwisho “Nyoni” ambalo ni jina la ukanda wa Sub Sahara [ Zambia, Zimbabwe, Malawi, Tanzania na Botswana]

Uhalisia ni kwamba Nyoni amezaliwa Uingereza lakini wazazi wake asili yao ni Zimbabwe

Baada ya bwana mdogo kuonekana jana Boniface Phiri akasema dogo ni wa Zambia na ilisambaa sana alipoandika “Zambia kuchalo” Zambia to the world] Zambia is well represented”.

Paul Jaguar Lewis akasema dogo ni wa kwao Malawi “All the way from Malawi”

Tanzania pia haikuwa nyuma Emanuel Warioba akasema “This boy is the future of Tanzania.”

Lakini asili ya dogo ni Zimbabwe na kama itatokea alashawishika kucheza timu ya Taifa ya Afrika basi atakipiga Zimbabwe

Chanzo: www.tanzaniaweb.live