Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dogo aliyelia kwa uchungu kumuona Ronaldo hatimaye akutana naye - VIDEO

Dogo Aliyelia Kwa Uchungu Kumuona Ronaldo Hatimaye Akutana Naye Dogo aliyelia kwa uchungu kumuona Ronaldo hatimaye akutana naye

Wed, 20 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mcheza soka maarufu wa klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia Cristiano Ronaldo alivutia idadi kubwa ya mashabiki alipowasili katika mji mkuu wa Iran siku ya Jumatatu kabla ya kuchuana na Persepolis, lakini miongoni mwa umati wa watu waliojitokeza nje ya hoteli yake pekee ni kijana mdogo aliyetambulika kwa jina Adrina.

Mashabiki hao walifurika nje ya hoteli hiyo kwa lengo la kumuona Ronaldo lakini hawakuweza kumuona na kijana huyo mdogo alionekana akilia kwa uchungu kwa kukosa nafasi muhali ya kukutana na mchezaji ambaye anampenda na kumuenzi.

Kwa mujibu wa jarida la Iran Front Page, Adrian, ambaye kilio chake nje ya hoteli ya Espinas Palace ya Tehran kwa kutoweza kukutana na Ronaldo kilisambaa, alitambuliwa na maafisa wa klabu hiyo ya Saudia na kupelekwa kwenye chumba cha mchezaji huyo.

Ronaldo alikuwa na mazungumzo ya kirafiki na Adrian, akampa shati yenye autograph yake na kupiga picha.

Kijana huyo alikuwa akivalia jezi ya Al-Nassr yenye jina la Ronaldo mgongoni na kuingizwa kwenye chumba ambacho supastaa huyo wa Ureno alikuwa akisubiriwa. Ronaldo alipiga picha na kusaini jezi ya mtoto huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live