Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma Jiji yatakata uwanja wa nyumbani

Dodoma Jiji (600 X 450) Kikosi cha Dodoma Jiji

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji Dodoma Jiji FC wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara,Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Mabao ya Dodoma Jiji yamefungwa na Khamis Mcha ‘Vialli’ dakika ya 37 kwa penalti na Emmanuel Martin dakika ya 59, wakati la Prisons limefungwa na Jeremiah Juma dakika ya tatu.

Dodoma Jiji wanafikisha pointi saba baada ya mechi nne na kusogea nafasi ya tatu wakizidiwa pointi mbili na Yanga na Polisi Tanzania ambazo zimecheza mechi tatu kila moja.

Tanzania Prisons inabaki na pointi moja baada ya kucheza mechi tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live