Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma Jiji yapiga hesabu kali VPL

09261316a1b9069e2630d506e94b0fa9 Dodoma Jiji yapiga hesabu kali VPL

Mon, 1 Mar 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

TIMU ya Soka ya Dodoma Jiji inapiga hesabu namna ya kushinda mechi zake zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara, VPL ili kumaliza nafasi za juu.

Moja ya malengo ya klabu hiyo ni kufanya vizuri kwenye ligi ikiwezekana kama sio kuchukua taji imalize nafasi nne za juu.

Akizungumza na gazeti hili kocha wa kikosi hicho Mbwana Makata alisema anashukuru kikosi chake hakijamwangusha kimekuwa kisikivu pale kinapopewa maelekezo ya kuzingatia katika kufanya vizuri.

“Tunahitaji kushinda mechi zetu zijazo ingawa kuna ushindani mkali, lakini naamini wachezaji wangu wakiendelea kufuata maelekezo ninayowapa watafanya vizuri na kutimiza yale tuliyokusudia,”alisema.

Makata alisema kila siku wanajipanga na wanaheshimu wapinzani wao wakijua kazi haitakuwa rahisi kutokana na umuhimu wa kila mmoja kuhitaji matokeo.

Alisema ni lazima wachukulie kila mchezo kama fainali ili wafike kule wanakotaka.

Dodoma Jiji kwa sasa inashika nafasi ya saba baada ya kucheza michezo 21, kushinda minane, kupata sare tano na kupoteza michezo minane ikiwa na pointi 29.

Timu hiyo imepanda kucheza Ligi Kuu msimu huu baada ya kufanya vizuri Ligi Daraja la Kwanza.

Chanzo: habarileo.co.tz