Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma Jiji yamtambulisha Zigah

Ziga Pic Data Dodoma Jiji yamtambulisha Zigah

Thu, 7 Jul 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kiungo Christian Zigar atakuwa  sehemu ya wachezaji wa kikosi cha Dodoma Jiji msimu huu  mara baada ya uongozi wa timu hiyo kumtambulisha rasmi leo.

Zigar hucheza namba sita na nane ni raia wa Ghana msimu uliopita aliitumikia  Biashara United ambayo imeshuka daraja na msimu huu  itacheza Championship   pamoja na Mbeya Kwanza.

Huu unakuwa usajili wa pili kwa Dodoma Jiji ambapo jana  ulimtambulisha mchezaji mwingine  raia wa Ghana Collins Opare kutoka timu ya Biashara United.

Mtendaji Mkuu wa Dodoma Jiji,Fortunatus John amesema mchezaji huyo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuwatumikia walima zabibu hao.

Miongoni mwa majina ambayo yanatajwa kusajiliwa na timu hiyo na wanaosubiri kutangazwa ni Jimmy Shoji kutoka Mbeya Kwanza, Amaan Kyata kutoka Coastal Union, Hassan Mwaterema kutoka Kagera Sugar, Randy Bangala na wengineo ambao majina yao wamefichwa.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz