Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma Jiji yaizamisha JKT

F44974d74faa2dc9f72d414772e8cf1f Dodoma Jiji yaizamisha JKT

Tue, 16 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

DODOMA Jiji FC ilijihakikishia pointi tatu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma jana.

Wenyeji Dodoma walipata ushindi kwa mabao yaliyowekwa kimiani na Khamis Mcha dakika ya tisa, bao la pili likipachikwa na Anuary Jabir dakika ya 81 huku wapinzani wao JKTwakipata bao la kufutia machozi dakika ya 51 na Edson Katanga.

Ushindi huo umewafanya Dodoma Jiji kufikisha pointi 25 na kushika nafasi ya nane kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 19 wakati wapinzani wao JKT Tanzania wakisalia nafasi 14 na pointi 20 wakishuka uwanjani mara 19.

Katika mchezo huo haukuwa na ushindani mkubwa kutokana na mazingira ya uwanja huo kujaa matope kwa baadhi ya maeneo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Mchezo ulianza kwa kasi kwa timu zote kucheza mpira wa kujihami zaidi na kushambuliana kwa zamu lakini kadri muda ulivyokwenda Dodoma walionekana kuwa bora.

Kipindi cha pili kilirejea kwa kasi kwa pande zote kufanya mabadiliko yaliyonekana kuwaongezea nguvu Dodoma eneo la kiungo waliendelea kutawala na kutengeneza mashambulizi kupitia pembeni.

Chanzo: habarileo.co.tz