Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma Jiji yaichapa Mtibwa Uhuru

Dodoma Jiji 1  0.jpeg Wachezaji wa Dodoma Jiji wakishangilia goli la ushindi

Sat, 30 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Mtibwa Sugar imeendelea kufanya vibaya katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya leo pia kuchapwa 1-0 na Dodoma Jiji FC bao pekee la Seif Abdallah Karihe dakika ya 61 Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Dodoma Jiji FC inafikisha pointi 10 baada ya mechi tano na kupanda kileleni, ikiizidi pointi moja Yanga ambayo hata hivyo ina mechi mbili mkononi, wakati Mtibwa Sugar wanabaki na pointi mbili katika mechi tano pia.

Bado kikosi cha Mcameroon Joseph Omog hakijaweza kuepuka matokeo yake ya misimu miwili iliyopita ambayo iliwafanya wajikute wanacheza hatua za Play Off.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live