Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma Jiji yachezea kwa Mtibwa

Mtibwa Sugar 123 Dodoma Jiji yachezea kwa Mtibwa

Mon, 18 Apr 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mtibwa Sugar imeondoka na alama zote tatu mara baada ya kuifunga Dodoma Jiji kwa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi kuu ya NBC uliochezwa katika uwanja wa Jamhuri Jijini hapa.

Mabadiliko yaliyofanywa na Mwalimu Djuma ya kuwatoa Habib Seif na Jamal Mtegeta na nafasi zao kuchukuliwa na Khamis Mcha na Hassan Maulid yaliipa uhai Dodoma Jiji katika  kipindi cha pili.

Hadi mapumziko ya dakika 45 za kipindi Cha kwanza Dodoma Jiji ilikuwa imekubali kichapo cha mabao 2-0.

Bao la Dodoma Jiji lilifungwa na Hamis Mcha kunako dakika ya 86 mara baada ya kupokea mpira uliopigwa na Hassan Maulid.

Kipindi Cha pili Mtibwa iliwatoa Nassoro Kiziwa, Ismail Mhesa, Ibrahim Ahmada na Said Ndemla  na nafasi zao kuchukuliwa na Baraka Majogoro,George Chota,Salum Kihimbwa  na Joseph Mkele.

Licha ya mabadiliko hayo lango la Mtibwa Sugar muda wote lilikuwa katika heka heka kutokana na Dodoma Jiji kutaka kusawazisha.

Kipindi Cha kwanza Makosa  ya Kipa wa Dodoma Jiji Rahim Sheikh na mabeki wake Joram Mgeveke na Nahodha Hamis Kibacha yalisababisha timu hiyo kuwa nyuma kwa mabao 2-0

Licha ya kushambulia kwa dakika zote 45 za kipindi Cha kwanza lakini umakini wa mabeki wa Mtibwa Dickson Daud na Oscar Masai umeweza kuzima mashambulizi yote ya Dodoma Jiji

Mtibwa walianza kupata bao kunako dakika ya 10 kufuatia kipa Rahim kuusindizia nyavuni mpira uliopigwa na Ismail Mhesa.

Goli la pili la Mtibwa liliwekwa kimiani kunako dakika ya 27 kupitia kwa Mayanja Mululi   kwa njia ya kichwa kufuatia Kibacha na Mgeveke kushindwa kuucheza mpira huo wa juu.

Kuona jahazi linazidi kuzama kunako dakika ya 36 Mwalimu wa Dodoma Jiji, Masoud Djuma alimtoa Anderson Kimweri na nafasi yake kuchukuliwa na Seif Karihe.

Dodoma Jiji iliongeza jitihaza za angalau kupata bao la kusawazisha lakini umakini wa Job na Masai ulizima ndoto za washambuliaji Anuary Jabir na Jamal na winga Mtegete.

Hadi filimbi ya mwamuzi Joachim Akamba Dodoma Jiji ilikubali kichapo Cha mabao 2-1 kutoka kwa Mtibwa Sugar.

Kwa matokeo hayo Dodoma Jiji ameendelea kubaki na pointi 21 huku Mtibwa akifikisha pointi 23.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz