Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma Jiji yaahidi ushindi dhidi ya Kagera Sugar

Dodoma Jiji Vs Mbeya CITY Dodoma Jiji yaahidi ushindi dhidi ya Kagera Sugar

Thu, 29 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Dodoma Jiji imetamba imejipanga kuondoka na pointi tatu katika mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar mtanange unaotarajiwa kupigwa saa 2:15 usiku katika uwanja wa Jamhuri Jijini hapa.

Dodoma Jiji ina pointi 10 inashika nafasi ya 12 kwenye msimamo ipo nafasi ya 18,imeshinda michezo mitano,imepoteza 10,sare mitatu,imefungwa mabao 23 na kufunga 12.

Mchezo uliopita ilikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Singida Big Stars mtanange uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Desemba 29 Jijini hapa Kocha wa timu hiyo,Kassim Liyogope amesema Kagera ni timu nzuri na inawachezaji wenye uzoefu lakini wamejipanga kupata matokeo.

“Timu yangu kwa sasa timu inatengeneza nafasi baada ya kuanza kupata matokeo lile tatizo la kutumia nafasi tumelimaliza.Changamnoto kubwa kwetu ni kuruhu mabao tumeifanyia kazi mechi dhidi ya Singida tulicheza vizuri tulipata nafasi tukashindwa kuzitumia.

“Tulikuwa na siku mbili za maandalizi tumezifanyia kazi kesho ‘Inshaalah’ ninaimani tutapata pointi tatu japo itakuwa ngumu kwa uwezo wa timu yangu naamini tutapata matokeo,”amesema Kocha huyo.

Kwa upande wake nahodha msaidizi wa timu hiyo, Augustino Nsata amesema wamejipanga kupata ushindi katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar

Chanzo: Mwanaspoti