Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma Jiji wana jambo lao Ligi Kuu

Dodoma Jiji Adhabu.jpeg Dodoma Jiji wana jambo lao Ligi Kuu

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Dodoma Jiji FC, umeweka wazi kuwa, kwa sasa kikosi chao kipo kwenye maandalizi ya kuwaanda wachezaji kuwaweka imara ili kupata pointi tatu katika mechi zijazo za Ligi Kuu Bara.

Mchezo uliopita, Dodoma Jiji walipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Tabora United.

Ofisa Habari wa Dodoma Jiji, Moses Mpunga, amesema: “Ushindani ni mkubwa na tunatambua kwamba tulianza vibaya kwenye ligi, lakini tunajua tuna kikosi bora ambacho kitatupa matokeo mazuri kwenye michezo ijayo.

“Ishu ya pointi tatu ni suala la muda, tunaamini tutashinda na kurejea katika ubora wetu kwani wachezaji tulionao ni imara na wapo tayari kwa ushindani.

“Mashabiki waendelee kutuunga mkono na tunawahakikishia tutawapa burudani ya kutosha kwenye ligi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live