Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma Jiji waisubiri kwa hamu Azam FC

Dodoma Jiji Pic Kikosi cha Dodoma Jiji

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: Dar24

Uongozi wa Dodoma Jiji FC umetamba kukamilisha maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC ambao umepangwa kupigwa kesho Jumanne (Oktoba 03), Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Afisa Habari wa Dodoma Jiji, Moses Mpunga, ameweka wazi kuwa, maandalizi ya mchezo huo yameshakamilika na wapo tayari kuikabili Azam FC katika mchezo huo wa mzunguuko wanne wa Ligi Kuu.

Akizungumza mjini Dodoma, Mpunga amesema: “Tumejiandaa vizuri, tunamshukuru Mungu kila kitu kinaendelea vizuri, tunahitaji pointi tatu, tunajua mchezo utakuwa mgumu, lakini tupo tayari kwa ajili ya kupambana.

“Hali ya wachezaji kwa ujumla ipo vizuri, hakuna majeruhi yeyote, wachezaji wetu wana ari na morali kwa ajili ya mchezo huo, wamejipanga vizuri kwa ajili ya kusaka alama tatu kwani wanajua nini tunataka kwenye mchezo huu.”

Chanzo: Dar24