Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma Jiji waichapa Ruvu Shooting

Dodoma Jiji X Ruvu Dodoma Jiji waichapa Ruvu Shooting

Sat, 3 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Dodoma Jiji imeendeleza makali yake hii leo walipokuwa nyumbani baada ya kuitungua timu ya Ruvu Shooting kwa mabao 2-1 kwenye mchezo ambao ulipigwa majira ya saa nane mchana.

Baada ya ushindi huo Walima zababu wao wamepanda hadi nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi wakiwa tayari wamecheza michezo 15, wameshinda michezo minne sare tatu na kupoteza michezo 8 pekee.

Huku Ruvu wao wakizidi kushuka baada ya kupoteza michezo minne mfululizo, wamepata ushindi michezo mitatu, sare mbili na kupoteza michezo kumi mpaka sasa kwenye Ligi.

Dodoma Jiji mchezo unaofuata wanatarajia kukipiga dhidi ya Mbeya City ya Mbeya ambapo watasafiri hadi Sokoine, huku Ruvu wao watamkaribisha Ihefu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live