Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma Jiji vs Simba, mechi ya kushuka na kubaki Ligi Kuu

Simba Vs Dodoma Jiji Leo Dodoma Jiji vs Simba, mechi ya kushuka na kubaki Ligi Kuu

Fri, 17 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dodoma Jiji vs Simba ni mechi nzuri sana kuitazama, Dodoma Jiji ikikutana na timu za Kariakoo mara zote huwa ni mechi ngumu tangu timu hiyo ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilipopanda daraja.

Ni mchezo muhimu kwa kila timu kutokana na nafasi wanazopigania kwa sasa. Dodoma Jiji ipo nafasi ya 11 ikiwa na alama 30 alama sawa na Singida Fountain Gate lakini Dodoma Jiji ina faida ya wastani wa magoli.

Kwa hiyo Dodoma Jiji bado haipo sehemu salama sana kwa sababu alama zake zinaweza kufikiwa na timu za chini yake kwenye msimamo [Mashujaa, Tabora United na Geita Gold] ambazo zipo kwenye hatari ya kucheza play offs au kushuka daraja.

Simba inahitaji alama tatu dhidi ya Dodoma Jiji kwa sababu ya kupigania kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo ili ishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Kwa hiyo ni mechi ambayo imekaa kimtego, Dodoma Jiji wanahitaji alama tatu ili kuondoka eneo la hatari ya kushuka daraja na kusogea juu ya msimamo lakini Simba wanahitaji alama zitakazo wasogeza kwenye kumaliza katika nafasi ya pili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live