Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma Jiji maji ya shingo

Dodoma Jiji Pic Dodoma Jiji maji ya shingo

Mon, 20 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ikijiwinda kwa mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Ihefu utajkaopigwa katikati ya wiki ijayo, timu ya Dodoma Jiji imekiri mambo ni mazito kwenye ligi kwa sasa wakati ikielekea ukingoni na kuahidi kumaliza msimu kwa heshima.

Dodoma inashika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa timu 16 ikiwa na pointi 24 baada ya kucheza mechi 23, ikishinda saba, sare tatu na kupoteza 13, huku ikifunga mabao 17 na yenyewe kufungwa 29.

Katika mechi saba ilizosalia nazo nne zitakuwa za nyumbani dhidi ya Ihefu, Polisi Tanzania, Coastal Union na KMC, huku tatu za ugenini kuvaana na Yanga, Namungo na Ruvu Shooting ambayo juzi ilitandikwa mabao 3-2 na Geita Gold ikiwa ugenini mkoani Geita.

Ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 2-1 na Mtibwa kwenye mchezo uliopita, Dodoma imesema inaanza msako wa pointi 12 za nyumbani kwa kuikaribisha Ihefu na kuhitaji ushindio kwa lengo la kujiweka pazuri kwenye msimamo kwani kwa sasa mambo yapo sivyo.

Kocha msaidizi wa Dodoma, Kassim Liyogope alisema wanaendelea na maandalizi kujiwinda na mchezo huo kuhakikisha wanabakisha alama tatu nyumbani.

Chanzo: Mwanaspoti