Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma Jiji kuja na siku maalum ya kutambulisha wachezaji

Dodoma Jiji Vs Mbeya CITY Dodoma Jiji kuja na siku maalum ya kutambulisha wachezaji

Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kikosi cha walima zabibu Dodoma jiji kuwatambulisha baadhi ya wachezaji, Mkurugenzi wa Jiji la Dodooma, John Kayombo amesema bado kuna wachezaji wa viwango vya kimataifa na majina makubwa wanatarajia kuwatambulisha hivi karibuni na hii ni kutokana na mipango ya kumaliza msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania Bara kwenye nafasi za juu.

Kayombo ameyasema hayo wakati akimtambulisha mdhamini mkuu wa timu hiyo PM BET ambapo amesema kwa sasa Dodoma Jiji huwezi kuifananisha na timu nyingine kutokana na usajili mkubwa walioufanya, maandalizi na mipango ya muda mrefu kuendelea kufanya vizuri na kushiriki michuano ya kimataifa.

"Tumetambulisha baadhi ya wachezaji tuliowasajili lakini kuna wachezaji wakubwa wa Kimataifa bado hatujawatambulisha bado na tunaendelea na usajili kwa sababu dirisha la usajili bado halijafungwa. Tunajipanga, tutakuja na siku maalum ya kutambulisha wachezaji wetu, tutawaambia ni lini.

"Timu imeshaanza maandalizi huko Arusha na hivi karibuni tutacheza mechi kama tano za maandalizi kabla ya msimu kuanza lakini tutakuwa na siku maalum ya kutambulisha wachezaji. Dodoma Jiji FC tumefanya maandalizi makubwa kwa sababu tuna malengo makubwa kwa msimu unaokuja," amesema Kayombo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live