Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma Jiji: Tutakuja kivingine 2023/24

Dodoma Jiji Jamhuri Dodoma Jiji: Tutakuja kivingine 2023/24

Mon, 3 Jul 2023 Chanzo: Dar24

Baada ya kumaliza ligi ikiwa nafasi ya tisa na alama 37 Klabu ya Dodoma Jiji imeweka wazi kuwa itaongeza nguvu katika kikosi hicho kwa msimu mpya.

Timu hiyo imeshuhudia ukuta wake ukiruhusu mabao 37 na safu ya ushambuliaji ilitupia mabao 26 baada ya kucheza mechi 30.

Afisa Habari wa Dodoma Jiji, Moses Mpunga amesema kuwa baada ya kukamilisha msimu wanaanza maandalizi ya msimu mwingine.

“Tayari msimu umeisha hilo tunashukuru licha ya kwamba kulikuwa na ushindani mkubwa na kila mmoja ameona namna hali ilivyokuwa, hivyo ambacho tunakifanya kwa sasa ni kusuka upya kikosi chetu.

“Shukrani nyingi kwa mashabiki kwa kuwa wamekuwa pamoja nasi kwa muda mrefu kwenye kila mechi na sasa tumemaliza msimu tunaanza maandalizi ya msimu mpya.

“Kwenye upande wa usajili tayari tumepitia ripoti ya usajili ambayo itafuatwa kwenye kila idara tutafanya kazi kwa umakini hilo linawezekana kikubwa mashabiki wasiwe na mashaka,” amesema Mpunga.

Chanzo: Dar24