Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma Jiji, Polisi TZ hakuna mbabe

Dodoma Jiji X Polisi.jpeg Dodoma Jiji, Polisi TZ hakuna mbabe

Tue, 1 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Polisi Tanzania imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

Kiungo Iddi Kipagwile alianza kuifungia Polisi Tanzania dakika ya 52, kabla ya Collins Opare kuisawazishia Dodoma Jiji FC dakika ya 90 na ushei, mabao yote yakipatikana kwa njia za penalti.

Timu zote zinafikisha pointi sita baada ya sare hiyo, Dodoma Jiji katika mchezo wa tisa na inasogea nafasi y 15 na Polisi katika mchezo wa 10 na inasogea nafasi ya 14.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live