Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma Jiji, KMC mechi iliishia katikati

Kati Kati KMC DOM Dodoma Jiji, KMC mechi iliishia katikati

Fri, 28 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Achana na ushindi ilioupata Dodoma Jiji dhidi ya KMC raha ilikuwa kuangalia ‘bato’ la katikati ya uwanja kati ya Baraka Majogoro na Emmanuel Mviyekure wa KMC na Salmin Hoza na Mwana Kibuta wa Dodoma Jiji.

Mchezo huo ulimalizika kwa Dodoma Jiji kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa dakika ya 19 na Mghana Collins Opare kwa shuti kali mara baada ya kupokea pasi mpenyezo kutoka kwa Rashid Chambo.

Huo ni mchezo wa mwisho kwa Dodoma Jiji kucheza nyumbani, michezo inayofuata itacheza ugenini dhidi ya Yanga, Namungo na Ruvu Shooting.

Dodoma Jiji inashika nafasi ya 10 ikiwa na pointi 31 huku KMC ikiendelea kubaki nafasi ya 14 ikiwa na pointi 26, timu zote zikiwa zimecheza michezo 27. Bato lenyewe lilikuwa hivi kila akigusa mpira Hoza ilikuwa lazima Majogoro awe amefika na kucheza faulo hivyo hivyo kwa Kibuta na Mviyekure.

Kutokana na hali hiyo mwamuzi wa mchezo huo, Julius Mnyupe kutokea mkoani Morogoro alimpa Majogoro kati ya njano kwa kumchezea faulo Hoza.

Kocha Msaidizi wa Dodoma Jiji, Kassim Liyogope alisema mchezo huo ulikuwa na ushindani wa hali ya juu na mechi iliamuliwa katikati ya uwanja.

Kocha Msaidizi wa KMC, Khalid Adam alisema licha ya kupoteza mchezo huo lakini wachezaji wake walicheza vizuri na wanajipanga kwa michezo iliyobaki.

Chanzo: Mwanaspoti