Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma Jiji FC yamnasa golikipa wa Kagera Sugar

Alain Ngeleka Golikipa Alain Ngeleka.

Tue, 9 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Dodoma Jiji iko mbioni kumsaji kipa wa Kagera Sugar raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Alain Ngeleka, ambaye alionyesha uwezo mkubwa msimu uliopita wa Ligi Kuu.

Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa kipa huyo aliomba kuondoka na kuvunja mkataba licha ya kwamba ulikuwa unamalizika 2025.

"Hakuna shabiki yeyote wa kweli wa soka ambaye hajamuona kipa huyu. Ni kipa mzuri sana kutoka DR Congo, kusema kweli atatusaidia sana, na huu ni ushauri wa kocha wetu Mecky Mexime kwa sababu ameshaifundisha Kagera Sugar," alisema mtoa taarifa ndani ya klabu hiyo, ambaye amebainisha watawatangaza rasmi hivi karibuni.

Klabu hiyo pia imewaongeza mikataba wachezaji wake 10, ambao imeona wanaweza tena kuisaidia timu hiyo kwa msimu ujao wa mashindano.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo, imeeleza wachezaji hao wataunganika na wale ambao itawasijili kwa ajili ya kuunda kikosi imara msimu ujao.

Wachezaji ambao wataendelea kusalia kwa 'Walima Zabibu' hao ni Yassin Mgaza, Fadhili Mwinyimvua, Emmanuel Martin, Zidane Sereli, Augustino Nsata, Anderson Kimweri, Robison Kamura, Ntenje Albano, Apollo Onyango, na Mwana Kibuta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live