Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma Jiji, Coastal hakuna mbabe

Coastal Vs Dom.jpeg Dodoma Jiji, Coastal hakuna mbabe

Mon, 10 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Dodoma Jiji na Coastal Union ya Tanga umelizika usiku wa jana katika uwanja wa Jamhuri,kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1.

Coastal Union walikuwa wakwanza kupata bao dakika ya 48 kupitia kwa mshambuliaji Maabad Maulid akiunganisha kwa kichwa krosi ya Vicent Abubakari.

Dodoma Jiji walizawazisha dakika ya 87 kupitia kwa Raizin Hafidh kwa shuti la karibu ambalo lilimshinda kipa wa Coastal Union Justin Ndikumana.

ZIFUTAZO NI DONDOO MUHIMU ZA MCHEZO HUU

Katika mechi sita (6) za msimu wa 2020-2021,2021-2022 na 2022-2023 Dodoma Jiji imeshinda mbili huku Coastal Union ikishinda moja (1) na zimetoka suluhu mara mbili (2) na sare ya Leo ya bao 1-1 Kocha wa Dodoma Jiji Melis Medo amewahi kuifundisha Coastal Union katika msimu wa 2021-2022 na baadae alitupiwa virago na nafasi yake ilichukuliwa na Juma Mgunda ambaye kwa sasa ni Kocha Msaidizi wa Simba.

Wachezaji wa Dodoma Jiji,Rashid Chambo,Amani Kyata,Mbwana Kibacha,Muhsin Makame wamewahi kuichezea Coastal Union kwa vipindi tofauti.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliofanyika katika uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga,Dodoma Jiji iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lilofungwa na Rashid Chambo kwa shuti kali.

Huu ni mchezo wa kwanza kwa Rehan Kibingu katika Ligi Kuu Bara, tangu ajiunge na walima Zabibu hao katika dirisha dogo la usajili.

Hii ni sare ya pili mfululizo kwa Coastal Union ambapo mchezo uliopita ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Singida Big Stars katika uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.

Miraji Abdallah aliumia dakika ya 60 na nafasi yake ilichukuliwa na Hamad Majimengi ambaye alikuwa mwiba mkali kwa mabeki wa Dodoma Jiji.

Kinara wa mabao katika timu ya Dodoma Jiji ni Collis Opare mwenye mabao sita huku Fiston Mayele wa Yanga akiongoza akiwa na mabao 15 akifuatiwa na Moses Phiri mwenye mabao 10.

Katika mchezo huu mwamuzi Abdallah Mwinyimkuu wa Singida aliwaonyesha kadi za njano Rehan Kibingu wa Dodoma Jiji na Greyson Gerrald,Yusuph Jamal

Mshambuliaji wa Dodoma Jiji,Collins Opare amepiga mashuti manne,mawili yamelenga goli(on target)na mawili yakitoka nje ya lango( off target).

Chanzo: Mwanaspoti