Mon, 29 Nov 2021
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/2022 imeeandele usiku wa jana kwa mchezo mmoja wa mzunguko wa saba kule Jijini Dodoma.
Wenyeji, Dodoma Jiji FC wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa Jumapili Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Kwa sare hiyo ya bila kufungana, Dodoma Jiji wanafikisha pointi 12 na kurejea nafasi ya tatu, wakati Coastal Union inatimiza pointi nane na kusogea nafasi ya saba baada ya wote kucheza mechi saba.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live