Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma FC sasa yatamba kutambulisha wa kimataifa

Dodoma Jiji Freeeesh Dodoma Jiji.

Mon, 29 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, John Kayombo, amesema bado kuna wachezaji wa viwango vya kimataifa na majina makubwa wanatarajia kuwatambulisha hivi karibuni.

Kayombo alisema mipango yao ni kumaliza msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye nafasi za juu ndio maana wanafanya usajili wa wachezaji wenye viwango vya kimataifa.

“Kwa sasa Dodoma Jiji huwezi kuifananisha na timu nyingine kutokana na usajili mkubwa tulioufanya, tupo kwenye maandalizi na mipango ya muda mrefu kuendelea kufanya vizuri ili tushiriki michuano ya kimataifa,” alisema Kayombo.

Kayombo pia alimtambulisha mdhamini mkuu wa timu hiyo, PM BET na kusema wameingia mkataba wa mwaka mmoja, ambao utaanza rasmi mapema msimu mpya wa Ligi Kuu 2024/25 utakapoanza.

Tayari Dodoma Jiji wamemtambulisha kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajibu kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Coastal Union ya Tanga, beki wa kati wa kimataifa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Heritier Lulihoshi, Dickson Mhilu na kipa Alain Ngeleka kutoka Kagera Sugar na Reliants Lusajo wa Mashujaa waliopewa mkataba wa miaka miwili.

Pia, ina benchi linaloongozwa na Kocha Mkuu, Mecky Maxime, Kocha Msaidizi, Nizar Khalfan na kocha wa makipa, Manyika Peter.

Aliahidi kuingia na ushindani kwenye kila mchezo watakaocheza kwa lengo la kuwapa burudani mashabiki pamoja na wadau wa soka mkoani humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live