Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk. Tulia amfuata Sugu

Sugu TuliaWA0088 Dk. Tulia na Sugu

Wed, 19 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Spika wa Bunge la Tanzania Dk Tulia Ackson ametoa Sh2 milioni kwa timu ya Mbeya City ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya timu hiyo kuelekea mchezo dhidi ya Kagera Sugar Aprili 23

Fedha hizo zimetolewa leo Aprili 18, 2023 wakati wa Chakula cha mchana kilichoandaliwa na Spika kwa wachezaji wa Mbeya City jijini Dodoma wakiwa safarini kuelekea Bukoba kwa ajili ya mechi itayochezwa uwanja wa Kaitaba

Akikabidhi zawadi hiyo kwa niaba ya Dk Tulia, mbunge Lupa Chunya Masache Kasaka kwa kushirikiana na wabunge wa Mbeya nao wametoa Sh1 milioni na kufanya jumla kuwa Sh3 milioni.

Wabunge hao pia wameahidi kununua ushindi kwa timu ya Mbeya City kwa kila mechi zilizosalia kwenye ligi Kuu ya Tanzania inayoendelea

Hivi karibuni Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' aliahidi kutoa Tsh Milioni 1 kwa kila bao la ushindi litakalofungwa na Mbeya City katika mechi zilizobaki

Mbeya City inashika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC ikiwa na alama 27 ikiwa ni alama saba juu ya eneo la kushuka daraja

Hata hivyo kama watamaliza katika nafasi hiyo, watacheza play-off.

Ikumbukwe pia kuwa, Mbunge Sugu aliahidi kutoa Tsh milioni 1 kwa kila bao watakalofunga Mbeya City ikiwa kama hamasa ili waweze kufanya vizuri kusalia ligi kuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live