Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Ndumbaro: Tatizo la Simba ni Yanga na Azam FC

Damas Ndumbaro Ngumi Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro

Sun, 9 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro, ameipongeza Yanga kwa mafanikio makubwa, yaliyofanywa chini ya rais wa klabu hiyo, injinia Hersi Said, huku akichomekea kwamba tatizo lililopo Simba kwa sasa sio kama timu imeporomoka, ila ni kupanga kwa viwango vya Yanga na Azam FC.

Ndumbaro amesema Wanayangwa wajitahidi kumlinda injinia Hersi kwa mafanikio wa klabu yao na maendeleo ya mpira wa miguu nchini.

"Mafanikio hayamei kama udongo, isipokuwa yamejengwa na kuleta na watu, hivyo nimpongeze injinia na mdhamini wao GSM,Yanga imekuwa bora ndio maana iliweza kufika fainaliza Kombe la Shirikisho Afrika na isingenyimwa bao dhidi ya Mamelodi ingecheza fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika," amesema Ndumbaro.

Ndumbaro, ameingizia utani kwamba wakati Yanga ikifanya vizuri, klabu yake (Simba) ni kama bundi amehamia kwao, badala ya mafanikio miaka minne nyuma sasa kumekuwa na migogoro.

"Siamini kama Simba ni mbaya, isingefika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, shida ninayoiona ni ubora wa Yanga na Azam, hivyo ijifunze na ikajipange upya, shida ya Simba na Yanga mojawapo ikiwa vizuri nyingine inaibua migogoro, hivyo zinatakiwa kubadilika," amesema Dk Ndumbaro anayefahamika kuwa mnazo mkubwa wa Msimbazi.

Pia hakusita kuisifia fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) iliyochezwa Yanga dhidi ya Azam kwamba dakika 120, watu walikuwa hawatulii kwenye viti.

"Nilikuwepo uwanjani, nilikaa na injinia, muda wote alikuwa anapiga kelele, nikamwambia tulia dawa ikuingie, lakini yote kwa yote nampongeza kwa kuchukua ubingwa huo," amesema

Chanzo: Mwanaspoti